Star Tv

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Seneti, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili.

Katiba ya Kenya inataka sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia bungeni kutotawala katika nyadhifa za uteuzi, na kwa miaka 10 sasa wabunge ambao wengi ni wakiume, wameshindwa kupitisha sheria hiyo.

Hatua hiyo ya Jaji Mkuu inaungwa mkono na chama cha Mawakili nchini humo na idadi kubwa ya wabunge wanawake ambao ni asilimia 22 katika baraza la bunge la kitaifa na asilia 22 katika Bunge la Senate.

Jaji Maraga amesema wabunge na maseneta wamekwenda kinyume cha Katiba ya mwaka 2010 iliyowataka kutunga sheria hiyo.

Spika wa bunge la kitaifa, Justin Muturi ameiambia Televisheni ya nchi hiyo ya “The Citizen” kuwa, hatma ya Bunge hilo sasa ipo mikononi mwa rais Kenyatta.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.