Star Tv

Wenza hao Julio Mora na Waldramina Quinteros walioana mwaka 1941, kwa ndoa ya siri baada ya familia zao kutoidhinisha mahusiano yao, ambapo Bwana ana miaka 110 na Bibi miaka 104.

Ndoa yao, iliyoanza kwa siri imedumu kwa miaka 79 na wenza hawa kwa pamoja wameishi si chini ya miaka 215 kwa ujumla.

Julio Mora na Waldramina Quinteros wamekuwa pamoja kwa muda mrefu kuliko wenza wengine wengi walio hai.

Bwana mwenye miaka 110 na bibi 104 wametambulika kuweka rekodi ya dunia ya Guiness kwa wenza walio na umri mrefu zaidi duniani.

Wapenzi hao ni raia wa Ecuador, Ambapo Mora alizaliwa tarehe 10 mwezi Machi , mwaka 1910 na Bibi Quinteros tarehe 16 mwezi Oktoba mwaka 1915.

Kuna ndoa zenye umri mrefu ambazo Guiness inazitambua, lakini hakuna yenye wenza walio na umri mkubwa zaidi

Wapenzi hawa walioana mwaka 1942 katika kanisa la kwanza kujengwa mjini Quito, Uhispania: La Iglesia de El Belen.

Julio aliwakimbia wazazi wake na kwenda kumuoa mpenzi wake baada ya kutopata ridhaa ya familia na wanandoa hao wote wawili ni walimu ambao wamestaafu na wanaishi eneo katikati ya mji wa Quito, mji mkuu wa Ecuador.

Kwa pamoja wanaweza kukusanya watu wengi kutokana na uzao wao: wana watoto wanne walio hai, wajukuu 11, vitukuu 21 na kilembwe kimoja.

Mwanzoni mwa mwaka, mmoja wa wajukuu wao alisema kuwa wazee hao huenda wakawa miongoni mwa wenza walio na umri mkubwa duniani., Ndipo mtoto wao Cecilia akatuma nyaraka kwa Guiness kisha wakapata uthibitisho katikati ya mwezi Agosti.

Cecilia amebainisha kuwa wazazi wake wako timamu na wenye afya njema, ingawa afya yao ya akili ilitikiswa kutokana na janga la corona.

''Kwa mwezi mmoja wamekuwa tofauti, wamekuwa wenye huzuni, kwa kuwa wanakosa mikusanyiko ya familia,'' alisema.

Cecilia amesema wenza hao (wazazi wake) wanapenda kwenda kwenye jumba la sinema na maonesho wakiwa pamoja, Na baba yake huwa anafurahi sana kutazama runinga na kunywa maziwa, huku Mama yake, anapenda kitinda mlo (desserts) na kusoma magazeti kila asubuhi.

Aidha, alipoulizwa kama ana ushauri kwa wale wanaotamani kuishi maisha marefu, Bi Quinteros amesema: ''ninashauri kusema kweli. Usiseme uongo, uongo unaweza kuipoteza dunia.''

Awali waliokuwa wanashikilia rekodi ya kuwa wenza wenye umri mrefu walikuwa wakazi wa Texas Charlotte na John Henderson, ambao kwa pamoja walikuwa na jumla ya miaka 212 na siku 52.

 

Credits:BBC Swahili.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.