Star Tv

Watu wasiofahamika wamevunja Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Mbeya Mjini na kuteketeza kwa moto baadhi ya nyaraka muhimu za chama hicho zikiwemo fomu za wagombea ubunge wa viti maalumu.

Akizungumza na wandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, John Mwambigija, ameliomba Jeshi la Polisi moani humo kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwabaini waliohusika na tukio hilo huku akiwataka wanachama wa chama hicho kutolipa kisasi hata kama wanamfahamu aliyetekeleza tukio hilo.

Ripoti iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich O. Matei imebainisha kuwa; Mnamo tarehe 19.08.2020 majira ya saa 03:00 usiku huko Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya. Mtu / watu wasiofahamika walichoma moto nyaraka mbalimbali zilizokuwa ndani ya ofisi ya CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini iliyopo eneo hilo. Ofisi hiyo ni ya chumba kimoja ambacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo wamepanga kwenye nyumba ya ANNA ABEL.

Mbinu iliyotumika ni kuvunja kufuli la mlango wa ofisi, kuingia ndani kisha kutoa baadhi ya nyaraka ziilizokuwa kabatini, kuziweka sakafu na kisha kuzichoma moto. Nyaraka hizo ni pamoja na fomu za matokeo ya kura za maoni kwa wagombea nafasi ya Udiwani, viti maalum wanawake jimbo la Mbeya mjini ambazo zilitakiwa kusafirishwa leo tarehe 19.08.2020 kwenda Makao Makuu – Dar es Salaam .

Aidha vitu vingine vilivyochomwa moto ni pamoja na viti vinne vya plastiki na mlango mmoja wa kabati lililokuwa limehifadhi nyaraka hizo.

Ofisi hiyo haina ulinzi Thamani ya mali iliyoteketea bado kufahamika. Kiini cha tukio kinachunguzwa japo uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na hali ya kutoridhika kwa baadhi ya wajumbe/wagombea kuhusiana na matokeo ya kura za maoni za Viti Maalum naUdiwani.

Ufuatiliaji unaendelea ikiwa ni pamoja na msako wa kuwakamata wahusika kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, hili ni tukio la pili kuripotiwa la aina hii ambapo usiku wa kuamkia Agosti 14, 2020 Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini za Arusha Mjini ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo hakikujulikana.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.