Star Tv

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba chanjo iliyotengenezwa ndani ya Urusi kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19 imeidhinishwa kwa matumizi baada ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu chini ya miezi miwili.

Bwana Putin amesema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vilivyowekwa na kuongeza kwamba binti yake mmoja tayari amepatiwa.

Maafisa kutoka nchini humo wamesema kuwa wana mpango wa kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma kuanzia Oktoba.

Wataalamu wameonesha wasiwasi wao kuhusu kasi ya kazi ya Urusi na kusema kuwa watafiti huenda wametumia njia za mkato.

Huku wasiwasi ukiendelea kuhusu uwezekano wa usalama kuingiliwa wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitaka Urusi kufuata miongozo ya kimataifa ya kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Chanjo iliyotengenzwa na Urusi sio miongoni mwa orodha ya zile za WHO ambazo zimefika awamu ya tatu ya majaribio kunakohusisha majaribio kwa watu wengi zaidi.

Akiitaja chanjo hiyo kuwa ya kwanza Duniani, Rais Putin amesema chanjo iliyotengenezwa na taasisi ya Moscow ya Gamaleya, inatoa "kinga endelevu" dhidi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Mikhail Murashko amesema chanjo hiyo imethibitisha kuwa salama na yenye ufanisi", na kupongeza kwamba ni hatua kubwa kuelekea ushindi kwa mwanadamu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Wiki iliyopita, Serikali ya Urusi ilitangaza kwamba inajitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma baada ya majaribio yake kufanikiwa, huku zaidi ya chanjo 100 kote duniani zinaendelea huku baadhi zikifanyiwa majaribio.

Licha ya maendeleo hayo yaliyopigwa kwa haraka, wataalam wengi wanafikiria kwamba chanjo hiyo haitakuwa inapatikana kwa wingi hadi katikati ya 2021.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.