Star Tv

Rais John Magufuli amesema Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alipenda nyumbani kwao Masasi ndiyo maana alikataa kuzikwa katika eneo lililotengwa jijini Dodoma kwa ajili ya viongozi wa ngazi za juu za serikali.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Julai 29, 2020, katika Kijiji cha Lupaso, Masasi mkoani Mtwara wakati wa maziko ya Mzee Mkapa.

“Tulipangiwa kuzikiwa Dodoma. Mzee Mkapa akaniuliza, ‘Mlipanga maziko yawe Dodoma? Mimi msinizike Dodoma.’ Nikasema, ‘wewe unataka wakuzike wapi?’ Akasema Lupaso. Nikamuuliza Mzee Kikwete akasema ‘mimi mnizike Msoga’, Mimi nilisema nitazikwa Chato. Niliogopa kumuuliza Mwinyi azikiwe wapi kwa sababu alikuwa na miaka zaidi ya 90, nikaona nikimuuliza halafu likatokea la kutokea nitaonekana mimi nimemletea uchuro, nikaona hilo eneo labda atazikiwa Mzee Malecela kwa sababu ni wa hukohuko Dodoma. Kwa sababu hakuna anayetaka kuzikwa Dodoma lile eneo nikaamua kuwapa wananchi na tayari walishaanza kujenga."-Rais Nagufuli.

Aidha, akizungumzia mazishi ya Mzee Mkapa, Rais Magufuli amewashukuru viongozi wa dini, Serikali na Watanzania kwa kushiriki kikamilifu kuupumzisha mwili wa kiongozi huyo mstaafu katika makazi yake ya milele.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.