Star Tv

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tundu Lissu hii leo amezungumzia kuhusu hatari anayoiona mbele yake wakati huu akitarajia kurejea nchini Tanzania.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao akiwa ughaibuni, kuhusu safari yake yakurudi nchini anayoitarajia hivi karibuni na wasiwasi alionao kuhusu usalama wake.

''Wale waliokuja kuniua hiyo siku ya tarehe saba Septemba miaka mitatu iliyopita na waliowatuma au waliowalipa au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana, maana yake ni kwamba hao watu bado wapo na kwa sababu bado wapo na hawajasema kama lengo lao la kuniua wameliacha, bado kuna hatari juu ya maisha yangu.Kwa hiyo ninarudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu haijaondoka bado. Lakini ninarudi tu, ni nyumbani kwetu, inabidi nirudi,"-amesema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu, katika miezi sita iliyopita, uongozi chini ya Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe aliandika barua mbili kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania, ili kuomba apatiwe ulinzi atakaporudi.

Amesema hadi sasa anasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ndio wenye jukumu la kuhakikisha kuwa yuko salama atakaporejea nchini humo.

"Naomba niseme hili kwa ajili ya kumbukumbu, mimi sina na siwezi kuwa na jeshi binafsi la kunilinda, sina na siwezi kuwa na rafiki au taasisi au nchi, ''Hata kutujibu barua tu kusema kuwa tumepokea barua yenu tunaifikiria, hawajafanya hivyo."

Lissu anatarajiwa kurejea Julai 28 akiwa mmoja wa wanaoomba kuteuliwa na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Latest News

RAIS TRUMP AKUTANA NA RUNGU LA UDHIBITI KUTOKA FACEBOOK NA TWITTER.
06 Aug 2020 12:53 - Grace Melleor

Mitandao ya kijamii Facebook na Twitter imemuadhibu Rais Donald Trump na kampeni yake kwa kutuma ujumbe ambapo rais huyo [ ... ]

KUMBUKIZI YA SHAMBULIZI LA BOMU LILOWEKA HISTORIA KUBWA DUNIANI.
06 Aug 2020 12:18 - Grace Melleor

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

KESI YA WAKILI SANGA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BADO NI KITENDAWILI.
05 Aug 2020 18:14 - Grace Melleor

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.