Star Tv

Kwa mara ya kwanza katika historia, rais wa Gabon, Ali Bongo, amemteua mwanamke, Christiane Ossouka Raponda kuhudumu kama waziri mkuu katika serikali. Ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kwenye nafasi hiyo, baada ya miaka 60 baada ya uhuru wa nchi hiyo.

Rose Christiane Ossouka Raponda (56), sio maarufu nchini Gabon Na ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kama Waziri Mkuu, pia alikuwa mawanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa meya wa mji wa Libreville mnamo mwaka 2014.

Hata hivyo mwaka 2019, Rais Ali Bongo alimtengua kwenye wadhifa wake na kumteua kuwa waziri wa Ulinzi, wadhifa ambao alikuwa akishikilia hadi baada ya uteuzi wake kama Waziri Mkuu wa Gabon.

Rose Christiane Ossouka Raponda aliingia kwa mara ya kwanza madarakani mnamo 2012, Pia Rais Bongo alimteua kuwa Waziri wake wa Bajeti wadhifa uliomstahili, kwa sababu Rose Christiane Ossouka Raponda ni mchumi. ambaye amehitimu katika Chuo Kikuu cha Uchumi na Fedha nchini Gabon.

Wataalamuwa masuala ya siasa nchini Gabon wanasema kazi yake kubwa kama Waziri Mkuu itakuwa ni kufufua uchumi na labda kufanya maandalizi ya uchaguzi ujao wa urais uliopangwa kufanyika mwaka 2023.

Latest News

RAIS TRUMP AKUTANA NA RUNGU LA UDHIBITI KUTOKA FACEBOOK NA TWITTER.
06 Aug 2020 12:53 - Grace Melleor

Mitandao ya kijamii Facebook na Twitter imemuadhibu Rais Donald Trump na kampeni yake kwa kutuma ujumbe ambapo rais huyo [ ... ]

KUMBUKIZI YA SHAMBULIZI LA BOMU LILOWEKA HISTORIA KUBWA DUNIANI.
06 Aug 2020 12:18 - Grace Melleor

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

KESI YA WAKILI SANGA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BADO NI KITENDAWILI.
05 Aug 2020 18:14 - Grace Melleor

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.