Star Tv

Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mwanasiasa na Mwanadiplomasia mbobezi Bernard Membe ni rasmi sasa, amejiunga na chama cha upinzani ACT- Wazalendo.

 Uanachama wake mpya katika ACT- Wazalendo umetangazwa leo na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe katika mkutano wa wanahabari wadau wengine kutoka ulimwenguni kote uliofanyika katika mtandao wa Zoom.

 Membe amesema amejiunga kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile

"Kilichonivutia katika chama cha ACT-Wazalendo ni katiba ya chama hicho na itikadi yake ya kutaka kuleta mabadiliko," amesema Membe

 Aidha bwana Zitto Kabwe amemtia moyo Membe kuchukua fomu kuwania nafasi ya uongozi ;"Watanzania watafurahia uchaguzi huu ujao," ameahidi Membe.

Kuhusu vyama vya upinzani kuungana na kuweka mgombea urais mmoja, Kabwe alisema mazungumzo baina ya vyama bado yanaendelea.

Kesho Julai 16 Membe atazungumza na Wanachama wa ACT-Wazalendo katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, huku taarifa zikieleza kuwa atatangaza kugombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Latest News

KUMBUKIZI YA SHAMBULIZI LA BOMU LILOWEKA HISTORIA KUBWA DUNIANI.
06 Aug 2020 12:18 - Grace Melleor

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

KESI YA WAKILI SANGA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BADO NI KITENDAWILI.
05 Aug 2020 18:14 - Grace Melleor

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.

“NASIKITISHWA NA MAMBO YASIYO YA BUSARA WANAYOFANYA CHADEMA”-Polepole
05 Aug 2020 12:54 - Grace Melleor

Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema amesikitishwa na kitendo kilichofany [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.