Star Tv

Upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi la awali mahakamani kupinga maombi yaliyowasilishwa na wadhamini Ibrahim Ahmed na Robart Katula wa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ukidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kutaka maombi hayo yatupwe.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wadhamini hao wamefungua maombi wakiitaka itoe hati ya kumkamata Lissu kwa kuwa wao wameshindwa kumpata.

Kesi hiyo imetajwa jana katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba maombi hayo kutupiliwa mbali kwa sababu mahakama hiyo haiwezi kushughulikia jambo hilo.

Alidai kuwa kupitia hati ya kiapo kinzani mahakama hiyo haiwezi kusikiliza na kutolea uamuzi wa maombi hayo ya walalamikaji na yatupwe.

Walalamikaji wanaomba mahakama itoe hati ya kumkamata Lissu kwa kuwa wameshindwa kumpata na kumfikisha mahakamani hapo.

Hati ya pingamizi la awali, iliwasilishwa mahakamani na Wankyo kwa sababu ndiye aliyepewa mamlaka ya kuendesha kesi ya msingi na maombi hayo.

Maombi hayo, yalipangwa jana mbele Hakimu Simba kwa ajili ya kusikiliza.

Hata hivyo, Wankyo aliomba mahakama itoe siku 14 ili aweze kujibu maombi hayo kwa njia ya maandishi.

Wankyo alidai kuwa anaomba siku hizo ili aweze kupitia jalada la kesi ya msingi na pia kupitia kesi mbalimbali ambazo zilishatolewa uamuzi.

Mmoja wa wadhamini hao (Katula), aliomba muda wa kujibu pingamizi hilo na hakimu alisema kisheria pingamizi la awali ndiyo linatakiwa kuanza kusikilizwa.

Hakimu Simba aliwauliza wadhamini hao kama wanapingamizi na suala la upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu yao kwa njia ya maandishi na waleta maombi walidai kuwa hawana pingamizi.

Alisema upande wa Jamhuri unatakiwa kuwasilisha majibu hayo Julai 28, 2020, Na waleta maombi wanatakiwa kujibu hoja hizo Agosti 11, 2020, kama kuna majibu ya ziada yatawasilishwa Agosti 18, 2020 na kesi itatajwa Agosti 19, mwaka huu na kupangwa tarehe ya uamuzi.

Wankyo alidai katika majibu yake hati ya kiapo kilichowasilishwa mahakamani na waleta maombi hao kuwa Lissu aliruka dhamana toka tarehe ambayo alipona na kutoka hospitali.

Aidha, alidai kuwa wadhamini hao walikuwa na taarifa za kutosha mahali alipo kwa sababu ilitangazwa na alieleza hivyo hivyo mahakamani, kwamba wadhamini wa mshtakiwa namba mbili (Lissu) wana wajibu wa kuhakikisha kwamba anafika mahakamani kwa mujibu wa amri ya mahakama iliyotolewa Januari 20, mwaka huu na hakimu Simba.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.