Star Tv

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, kuwa mgombea wa Urais wa Tanzania, kwa asilimia 100 leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020.

“Nilipomteua Mama Samia kuwa Makamu wa Rais mwaka 2015 sikujua utendaji kazi wake vizuri lakini ni mchapakazi, anajituma pia ni mzuri, Wasukuma tunapenda weupe, ukiwa na Msaidizi mweupe hata ukiwa na stress zinaisha, nimeamua awe tena Mgombea mwenza wangu"-Rais Magufuli.

Aidha, Rais magufuli amesema amemteua mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza kwakuwa kipindi chote alichofanya naye kazi amejifunza mambo mengi: "nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa Wanawake, Mama Samia nikimtuma popote hakatai kama ilivyo nyie akina Mama mkitumwa hamkatai, nampa tena ugombea mwenza"-Amesema Rais Magufuli

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.