Star Tv

Wanafunzi watano wa darasa la kwanza katika  shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera  wamefariki na wengine 18 kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kurushwa kwa mkono asubuhi ya leo wakati wakiingia darasani.

Kwamujibu wa diwani wa kata ya Kibogora wilayani humo Adronis Bulindoli amesema kuwa kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu kiliwalipukia wanafunzi hao kabla ya kuingia darasani na wengine18 kujeruhiwa ambapo wamekimbizwa katika hospitali ya Misheni ya Rurenge kwa ajili ya kupata matibabu.

Aidha Bulindoli amesema kuwa waliofariki  wana umri kati ya  miaka 8 hadi 9 .Kati ya hao wanafunzi watatu, wamefariki pale pale huku wawili wakipoteza maisha wakiwa njiani wakati wakipelekwa hospitali ya Rurenge.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Ngara Erick Nkilamachumu amesema kuwa wauguzi wa hospitali ya Rulenge wanaendelea na jitihada za kuokoa maisha ya wanafunzi waliojeruhiwa wa kata za Bugarama na Kibogora ilipo shule ya msingi Kihinga.Shule ya msingi kihinga h iko  mpakani mwa nchi jirani ya Burundi ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanadai huenda bomu hilo lililetwa na wanafunzi wanaokuja shuleni kuuza vyuma chakavu.Aidha Mganga mkuu wa Hospitali ya Misheni Rulenge  Mariagolet Francis amekili kupokea wanafunzi 18 majeruhi na miili ya wanafunzi wawili walipoteza maisha wakiwa njiani kupelekwa hospitalini hapo.Kwa upande wa mkuu wa Wilaya hiyo Luten kanali Michael Mntenjele akiwa Wilayani Missenyi katika zira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Nimepigiwa simu kutoka Ngara nikaambiwa kwamba kuna tukio kitu kinachofanana na bomu kulipukia watoto na kutokea vifo ila sijajua ni wangapi wamejeruhiwa na vifo sijajua vingapi ila nimeagiza wataalam wangu waende kuona na kujilidhisha kama ni bomu,hivyo namie najiandaa kurudi Ngara kwa ajili ya tukio hilo kwahiyo nitatoa taarifa baadaye nikiipata taatifa kamili" alisema
Mntenjele.
Hadi sasa kwa taarifa zilizopo nikuwa vifo vimeongezeka kutoka 5 hadi kufikia 6 baada ya kufia hospital na majeruhi kutoka 18 hadi kufikia 24

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.