Star Tv

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura 129 sawa na asilimia 78.65 akiwashinda wenzake wawili Shamsi Vuai Nahodha na Dkt. Khalid Salim Mohamed.

Awali Katibu Mkuu wa Chama cha CCM Dkt.Bashiru Ally alitaja majina matatu kutoka majina matano yaliyokuwa yamepitishwa na Kamati Kuu Maalum kuwania nafasi ya urais Zanzibar. Majina hayo matatu yaliyokuwa yametajwa kupita ni Dkt. Hussein Mwinyi, Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Dkt. Khalid Salum Mohammed.

Dkt. Hussein Mwinyi ni miongoni mwa majina matatu yaliyotajwa leo Julai 10,2020 kwenye ufunguzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika katika ukumbi wa White House Dodoma na kupigiwa kura ndani ya ukumbi huo kutoka kwa viongozi mbalimbali ndipo Dkt.Hussein Mwinyi akatajwa kuibuka kidedea ambaye anatarajiwa kushindana na mgombea kutoka chama cha upinzani kuwania kiti cha Urais Zanzibar

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.