Star Tv

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (Tanzania) mwishoni mwa Julai ili kuhudhuria mkutano huo, ambapo katika Mkutano huo ndio utaamua kumpitisha nani atakayepata ridhaa ya kuwania urais mwaka huu kupitia Chama hicho.

Lissu amesema atarejea nchini kuendelea na shughuli za kisiasa, ambapo mpaka sasa yuko nje ya nchi kwa matibabu tangu septemba 2017 na hakuwahi kurudi nyumbani tangia mwaka huo alipoenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Tundu Lissu ni mmoja kati ya wagombea waliojitokeza kutia nia ya kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia. Wagombea wengine, huku baadhi ya wagombea wengine ni mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu.

 

Latest News

KUMBUKIZI YA SHAMBULIZI LA BOMU LILOWEKA HISTORIA KUBWA DUNIANI.
06 Aug 2020 12:18 - Grace Melleor

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

KESI YA WAKILI SANGA DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI BADO NI KITENDAWILI.
05 Aug 2020 18:14 - Grace Melleor

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam.

“NASIKITISHWA NA MAMBO YASIYO YA BUSARA WANAYOFANYA CHADEMA”-Polepole
05 Aug 2020 12:54 - Grace Melleor

Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema amesikitishwa na kitendo kilichofany [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.