Serikali imetoa utaratibu maalumu kwa watu wanaokwenda kupiga picha katika Daraja la Nyerere, Kigamboni
Serikali imetoa utaratibu maalumu kwa watu wanaokwenda kupiga picha katika Daraja la Nyerere, Kigamboni ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara, fedha zinazokusanywa, wapiga picha wenyewe, pamoja na kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.
Wapigapicha watalazimika kuomba kibali kwenye Ofisi Mkurugenzi Mkuu.
Gharama za upigaji picha kwa matukio maalumu (harusi, kwaya, wasanii) ni Tsh 250000 kwa saa moja.
Wanaopiga picha moja moja (selfie) hawatolipa, lakini wametakiwa kuchukua tahadhari ya usalama wao.