Star Tv

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai akiomba mahakama hiyo kutengua amri ya Spika kumtambua Cecil Mwambe kama mbunge halali wa Ndada ikisema amekosea kufungua shauri hilo.

Katika kesi hiyo Wakili Kaunda anaiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya Spika Ndugai ya kumtambua Mwambe kama Mbunge halali wa Ndanda.

Katika uamuzi mdogo uliosomwa leo Juni 3, 2020 na Jaji Issa Maige aliyekuwa akisaidiana na Jaji Stephen Magoiga na Jaji Seif Kulita amesema mlalamikaji alikosea namna ya kufungua kesi ya kikatiba badala yake alipaswa kufungua kesi kwa utaratibu wa kawaida.

Amesema, kauli ya Spika Ndugai aliyoitoa haikuwa imevunja katiba bali ni ya kiutaratibu katika shughuli zake za kiutendaji hivyo mlalamikaji angekuwa sahihi kama angefungua kesi hiyo kwa utaratibu wa kawaida kwa kutumia Ibara ya 83 (1) badala ya ile ya 26 (2) aliyoitumia.

Jaji Maige amesema Ibara hiyo inaenda sambamba na kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi ambacho kinaeleza kuhusu utaratibu wa kutangaza kiti cha Mbunge ambacho kiko wazi.

Wakili Kaunda alifungua kesi mahakamani hapo dhidi ya Ndugai, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo Wakili Kaunda anadai Mwambe alitangaza kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kauli ambayo iliungwa mkono na katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally aliyempokea rasmi Mwambe mbele ya hadhira kwa kumkabidhi kadi ya CCM, na Mwambe naye alimkabidhi Katibu Mkuu huyo kadi yake ya Chadema.

Wakili Kaunda anadai kitendo cha Spika kumtambua Mwambe kama mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini kama Mbunge wa Ndanda (2015-2020), ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na hakuna mamlaka yoyote nchini, achilia mbali Spika, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni Mbunge ambaye kwa hiyari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.