Star Tv

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kujitokeza kuanzia leo Juni 3 hadi Juni 15 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mnyika amesema taarifa za kusudio la kugombea urais kupitia chama hicho zinapaswa kuwasilishwa katika ofisi ya Katibu Mkuu na baadae zitajadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho na kutolewa uamuzi.

Kwa mamlaka niliyopewa na kanuni hii ya chama ninaomba kutangaza sasa tarehe za mwanzo wa zoezi hili na tarehe za mwisho wa zoezi hili la kutangaza nia ya kusudio la kugombea milango hii imefunguliwa kuanzia tarehe ya leo mpaka tarehe 15 ya mwezi Juni” amesema Mnyika

Licha ya suala hilo la kugombea nafasi ya urais Katibu Mkuu huyo pia amesema kuwa chama hicho kimefungua milango ya ushirikiano na vyama vingine kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na vyama ambavyo ameviita ni vyama makini.

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.