Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameagiza vyuo vyote nchini kufunguliwa Juni 01, 2020 pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita kufungua shule tarehe hiyohiyo kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya taifa, huku akisema shule za sekondari na msingi waendelee kusubiri.

Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo katika ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, ambapo amezitaka Wizara husika kama vile Wizara ya Fedha, Wizara ya elimu pamoja na nyinginezo kujiandaa kikamilifu kwakuwa zimebaki siku tisa kutokea leo hii.

Ametoa wito kwa Wizara ya Afya kuhakikisha inapima kikamilifu vifaa vinavyotolewa kama msaada nchini kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, na ikiwa mtu yeyote atapatikana amepokea vifaa ambavyo pindi vitakapopimwa vitakutwa na corona mtu huyo atapelekwa kwenye kesi ya jinai.

Mbali na kutangaza vyuo vyote kufunguliwa Juni 01, pia ligi za michezo zilizokuwa zikiendelea zitaanza tarehe hiyohiyo.

Amesema ni lazima watu wafanye michezo kwa kuwa hakuna ripoti yeyote inayoonyesha kuna mchezaji wa tanzania amefariki kwa COVID-19, lakini Wizara ya Afya nay a Michezo zitapaswa kupanga namna ya watu kushangilia michezo hiyo lengo ni kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwakuwa ugonjwa bado upo.

Viongozi walioapishwa leo ni; Dtk. Godwin Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake Wazee na watoto, Dkt. Deliphine Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Dkt. Jacob Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Mteule Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi mteule John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Brig.Gen.John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.