Star Tv

Ikiwa leo ni Siku ya Wauguzi Duniani, Wauguzi nchini wametoa rai kwa wauguzi wote walioko katika hospitali mbalimbali kuwa na kauli nzuri, upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia kwakuwa kauli ya muuguzi inaweza kumfariji mgonjwa pamoja na kuthamini utu wa wagonjwa.

Kwa upande wake Bilha Melita ambaye ni mwekahazina wa Chama cha Wauguzi Arusha ameiomba jamii kuacha kuwa na mtazamo mbaya kwa wauguzi kwakuwa wengi wao wamejirekebisha na kwasasa na hawatoi kauli mbaya kwa wagonjwa kama inavyosemekana isipokuwa kila mtu ana tabia zake.

Muuguzi aitwaye Sofia Sanga kutoka Dar es Salaam amefafanua kuwa kwa zama zimebadilika sio kama zamani na Muuguzi ni msaidizi wa wagonjwa na sio msaidizi wa daktari kama wengi wanavyodhani.

Makamu wa rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahimu Mgoo amesema Wauguzi wanajitahidi kufanya vyema kazi zao japo kuwa muda mwingine wanakumbana na hali ngumu ikiwemo uchache wao hususani katika kipindi hiki cha Ugonjwa huu wa COVID-19 na kuiomba serikali iliangalie suala hili.

Yote haya wameyazungumza kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na StarTv ambapo wote hao wamewataka wauguzi wote nchini kuitumia vyema taaluma yao namna inavyowapasa.

Aidha, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la afya WHO katika maadhimisho ya siku hii, umesema mchango wa wahudumu hawa wa afya hauna kipimo hasa wakati huu ambao janga la virusi vya corona linaitikisa dunia.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.