Star Tv

Kamati Kuu ya CHADEMA imewafutia uanachama wabunge wanne wa chama hicho ambao ni Anthony Komu, Joseph Selasini,David Silinde na Wilfred Rwakatare.

Kufutwa uanachama kwa wabunge hao ni kutokana na kile kilichoelezea na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa wamepoteza sifa ya uanachama wa Chama hicho.

Mnyika ameleeza kuwa Mbunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wamekuwa wakiuka maagizo ya Chama na hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama.

Amesema Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu kwamba wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, na hivyo kamati kuu ya CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama.

Pia amesema mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, na wakati alitakiwa awe mfano, Kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo.

Aidha, Mnyika amesema kuhusu Wabunge wengine ambao wamekwenda kinyume na maagizo ya Chama hicho lakini hawajaonyesha utomvu wa nidhamu kwa kutoa kashfa kwa Chama na watatakiwa kujieleza ni kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo ya Chama.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.