Star Tv

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amewasili nchini Madagascar kuchukua dawa ya Corona.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege nchini humo Waziri Kabudi alipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Mhe. Tehindrazanarivelo Djacoba.

Akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Mhe. Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Antananarivo Waziri Kabudi alionekana katika picha nyingine  anakabidhiwa maboksi ya dawa hizo.

Kufikia sasa watu 509 kutoka 480 ndio walioambukizwa ugonjwa wa corona  hapa nchini mara baada ya Wizara ya Afya ya Zanzibar hapo jana kutangaza wagonjwa wapya 29.

Mnamo Mei 3, Rais wa John Pombe Magufuli alisema kuwa atatuma ndege kwenda Madagascar kufuata dawa hiyo ya mitishamba, Japokuwa Shirika la Afya Duniani limesema ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu virusi vya corona kufanyiwa majaribio kwanza kabla ya kuanza kutumiwa.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.