Star Tv

Serikali imepanga kuweka utaratibu wa kisheria utakaowataka wawekezaji wa Viwanda,Mazao, Bidhaa na Huduma kutotumia nguvu ya soko kuwakandamiza wateja.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa bungeni leo Mei 05, 2020 jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa Bungeni wakati akiliwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa fedha 2020/2021.

Waziri Bashungwa amesema Wizara anayoiongoza imeweka malengo na mikakati madhubuti yakuhakikisha soko la uhakika nje ya nchi linakwenda vyema na bidhaa za Tanzania zinapasua mawimbi ndani na nje ya nchi.

Kilio cha Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulika na Viwanda, Biashara na Mazingira kwa muda mrefu ni mwenendo usioridhisha wa utoaji wa fedha za miradi ya maendeleo na baadhi ya Wabunge wameomba fedha zinazoombwa kwenye Wizara hiyo ni vyema zikatolewa mapema pasipo ubabaishaji ili kuendeleza Viwandana kuleta matokeo chanya kwa taifa.

Bunge limepitisha shilingi Bilioni 81. 36 ili Wiizara ya Viwanda na Biashara iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.