Star Tv

Jumla ya wagonjwa 18 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo katika kambi maalum ya upasuaji inayofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya New Delhi nchini India.

Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hiyo ya siku sita ni wa kufungua kifua kwa watu wazima.

Upasuaji utakaofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve).

Daktari bingwa wa Moyo na mishipa ya damu ambae pia ni Kaimu mkurugenzi wa Idara ya upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa amesema katika kambi hiyo  wanatarajia kufanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku

Dkt. Nyangasa amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi wanaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri na hivyo kuwashauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.

 Aidha Dkt. Nyangasa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu nyingi kati ya chupa 5 hadi 6.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.