Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Dkt. Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).

Uteuzi wa Brigedia Jenerali Dkt. Mhidize umefanywa Mei 03, 2020, kabla ya uteuzi huo Brigedia Jenerali Dkt. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.

Uteuzi huo mpya umejiri baada ya rais Magufuli kusema kuwa sampuli kadhaa ambazo hazikuwa za binadamu zilitumwa katika maabara ya taifa ili kupima ubora na usahihi wa majibu ya mashine hizo katika vipimo vya ugonjwa huo na kuleta majibu yaliyoacha maswali mengi kwakuwa sampuli hizo zilipewa majina ya binadamu na kupelekwa bila ya wataalamu wa maabara kujua kuwa si za bidanamu.

“Sampuli ya oili ya gari ilipewa jina la Jabiri Hamza na haikukutwa na corona. Sampuli ya Tunda la fenesi ilipewa jina la Sara Samuel majibu yake hayakukamilika, sampuli ya papai iliitwa Elizabeth na kukutwa na corona”-Amesema Rais Magufuli.

Alisema sampuli ya ndege aina ya Kware pia ilikutwa na corona pamoja na mbuzi.

"Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii, ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa," amesema Magufuli.

Magufuli amesema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wana maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Lazima kuna watu wameambiwa positive lakini si wagonjwa wa corona, na inawezekana wengine wakafa kwa hofu. Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza…kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita"

Aidha, rais Magufuli amesema kuwa amewasiliana na Madagascar baada ya kupokea barua rasmi kutoka nchi hiyo iliyoeleza kuwa wamegundua dawa ya corona na kusema kuwa atatuma ndege Madagascar kwenda kufuata dawa ya mitishamba ambayo rais wa nchi hiyo anadai kuwa inatibu corona.

Brigedia Jenerali Dkt. Mhidize amechukua nafasi ya Laurean Rugambwa Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo hii.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.