Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema mazishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda yatafanyika Mtwara na kuhudhuriwa na watu wasiozidi kumi tu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amesema lengo la watu kumi kuhudhuria mazishi ya Bwana Mmanda ni kuendelea kusimamia msimamo wa Wizara ya Afya juu ya kuzuia mikusanyiko katika kipindi hiki cha maambukizi ya Corona.
Mazishi ya Mkuu wa Wilaya huyo yatasimamiwa na serikali na tayari familia ya marehemu imeridhia mwili wa mwanafamilia wao kuzikwa mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa amesema Bwana mmandi alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo na Sukari ambapo hali yake ilibadilika siku ya Ijumaa na kulazwa katika hospitali ya Ligula.
Marehemu Evod Mmand, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo, ambapo alianza kuhudumu katika nafasi ya ukuu wa Wilaya mwaka 2016, baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe magufuli.