Star Tv

Waziri wa Afya nchini Ummy Mwalimu amesema kuwa mgonjwa mwingine aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini amepona.

Waziri Ummy ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Aprili 03, 2020 kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo akaunti ya Twitter ana Instagram.

Amesema kuwa mgonjwa huyo alikuwa Ngara mkoani Kagera amepona na kupona kwakwe mgonjwa huyo kunafikisha idadi ya waliopona Corona kuwa watatu.

Pia Waziri Ummy pia ameandika kupitia kurasa zake hizo kuwa “Mgonjwa aliyebaki Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative, Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wagonjwa wengine 15 waliobaki wanaendelea vizuri”.

Waziri Ummy ameendelea toa rai na kusisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo kwa kuepuka misongamano , mikusanyiko safari zisizo za lazima na pia kufuata maelekezo ya wataalam ili kujikinga na maambukizi ya COVID-19

                                           Mwisho.

Latest News

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

RAIS MAGUFULI AKABIDHI TAUSI 25 KWA MAMA MARIA NYERERE NA MARAIS WASTAAFU.
30 May 2020 09:49 - Grace Melleor

Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana I [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.