Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesema serikali yake itakamata mifugo itakayoingia nchini kutoka nchi jirani kinyume cha sheria.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera katika ziara yake ya kikazi na kuongeza kuwa Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani na mifugo hiyo ikikamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa na kuzitakata nchi jirani kufanya vivyo hivyo kwa mifugo ya Tanzania.

"Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani, ndio maana tumeamua kukamata mifugo na kuchukua hatua kwa mujibu wa kisheria, na hata huko kwenye nchi jirani wakishika mifugo ya kutoka Tanzania wachukue hatua za kisheria za nchi hizo" alisisitiza rais Magufuli.

Matamshi hayo ya Magufuli yanajiri wakati ambapo kumekuwa na mgogoro wa mpakani mwa Kenya na Tanzania kuhusu mifugo katika siku za hivi karibuni.

Wiki tatu zilizopita serikali ya Tanzania ilizikamata zaidi ya ng'ombe 1000 kutoka Kenya na baadaye mahakama moja nchini ikaamuru mifugo hiyo kupigwa mnada na fedha hizo kutumiwa na serikali iwapo wamiliki wa mifugo hiyo watashindwa kulipa faini ya shilingi milioni 500 za Tanzania.

Na wiki moja iliopita takriban ng'ombe 4000 kutoka Tanzania zilidaiwa kupatikana katika jamii moja ya Maasai mjini Kajiado. Hivi majuzi hatua ya taifa la Tanzania kuwachoma kuku 6,400 kutoka Kenya wenye thamani ya shilini milioni 12 za Tanzania kwa madai kwamba wangesambaza ugonjwa wa homa ya ndege ilizua hizo tofauti kutoka kwa watetezi wa wanyama .

Afisa mkuu wa maswala ya mifugo nchini Tanzania Obedi Nyasembwa alisema kuwa kuku hao waliingizwa nchini humo kinyume na sheria na kwamba uwepo wao nchini humo ulikuwa hatari kwa ndege wengine. Kuku hao wa siku moja walikamatwa katika eneo la Namanga huku mfanyabishara wa Tanzania akikamatwa.

Baadaye mamlaka ya Tanzania iliwamwagia mafuta na kuwachoma kulingana na gazeti la mwananchi.

Aidha rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Kagera kuhakikisha kuwa mifugo yao inawekwa alama kwa mujibu wa sheria, ili kurahisisha utambuzi wa mifugo inayoingizwa nchini kutoka nchi jirani na pia kudhibiti ruzuku inayotolewa na Serikali kwa dawa za mifugo za hapa nchini.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

KARATE: Rutashobya aomba serikali iruhusu Karate kufundishwa mashuleni
10 Dec 2019 12:32 - Grace Melleor

Bingwa wa Dunia wa Mchezo wa Karate Rutashobya Rwezahula¬† amesema Tanzania inaweza kutoa Mabingwa wengi katika Mchezo h [ ... ]

WANANCHI WANAOTOA NUSU YA FEDHA: Meneja TANESCO Pwani aagizwa kuwaunganishia ume...
10 Dec 2019 11:46 - Grace Melleor

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO mkoa wa Pwani¬†Martin Maduu ku [ ... ]

UKOSEFU WA MAFUTA MAALUM: Walemavu wa ngozi hatarini kupata Saratani
10 Dec 2019 11:38 - Grace Melleor

Walemavu wa Ngozi wanaoishi wilayani Monduli mkoani Arusha wapo hatarini kupata saratani ya Ngozi kutokana na kukosa maf [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.