Star Tv

Maafisa usafirishaji na wafanya biashara wadogo wa kituo cha mabasi Halmashauri ya mji wa Makambako wameiomba halmashauri kuchukua hatua za haraka kufanya ukarabati wa Kituo hicho, ili kuepusha hasara na mlipuko wa magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na ubovu wa miundombinu ya kituo hicho.

Taarifa na Dickson Kanyika

Madereva hao pamoja na Halmashauri ya mji wa Makambako wamesema hali ya miundombinu ya stendi hiyo hairidhishi wakati wanalipa ushuru kwa mamlaka husika.

Maafisa usafirishaji wanalalama kwamba halii imeendelea kuwapa hasara kutokana na magari yao kuharibika hali inasababisha kukosekana kwa maelewano baina ya madereva na waajiri wao.

Ndani ya Kituo hicho cha mabasi kinaelezwa  pia kuwepo na wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara za uuzaji wa vyakula na vinywaji ambao  wamesema hali ya usalama wa afya zao na watumiaji wa bidhaa wanazoziuza ndani ya kituo hicho si salama kutokana na kuwepo kwa  maji yaliotuama kwa muda mrefu yanayombatana na Harufu kali.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji huu wa Makambako Rashid Njozi Musa amekiri kuwepo kwa changamoto ya ubovu wa miundombinu, ambapo amesema yeye kama  kiongozi wa halmashauri wanashughulikia tatizo hilo na wanasubiri mvua zipungue ili ukarabati uweze kufanyika haraka iwezekanavyo.

                                   Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.