Star Tv

Upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu umeomba muda wa kutosha kupitia na kujibu maombi ya kujitoa kwa wadhamini wa makamu mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Taarifa na Angela Mathayo.

Maombi hayo yamewasilishwa  na wakili mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon.

Wakili huyo wa upande wa mashtaka ambaye ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kutokana na wadhamini wa Lissu kuwasilisha maombi hayo, hawakupata muda mzuri wa kuyapitia.

Wakati upande wa mashtaka ukiomba muda zaidi ili uweze kupitia maombi ya wadhamini hao, wakili wa Lissu aliiomba mahakama hiyo iahirishe kusikiliza maombi hayo hadi Februari 24, 2020.

Itakumbukwa kuwa februari 20 wadhamini wa aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiomba itoe kibali ili makamu mwenyekiti huyo wa CHADEMA kukamatwa.

Awali mahakama ilitaka kuwakamata wadhamini hao baada ya kushindwa kumpeleka waliyemdhamini mahakamani hapo.

Mmoja kati ya wadhamini wa Tundu Lissu, Robert Katula aliieleza Mahakama juhudi walizofanya kuhakikisha mshtakiwa anafika Mahakamani ikiwa ni pamoja na kumwandikia barua Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Katika kesi ya msingi Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati  Januari 12 na 14, 2016 jijini Dar es Salaam ambapo Jabir, Mkina na Lissu waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi.

                                                            Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.