Star Tv

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepata suluhisho la kudumu la kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima inayosababisha mauaji, wizi wa mifugo na mifugo ya nchi jirani kuingia nchini kwa ajili ya malisho kwa kupiga chapa mifungo katika eneo husika.

Mwanza ni moja ya mikoa ambayo wakazi wake kwa asili ni wafugaji na wakulima. Ufunguzi wa zoezi la upigaji chapa ya Taifa kwa Ng’ombe wa wilayani Sengerema mkoani Mwanza umezingatia kulinda ngozi ya Ng’ombe itakayowawezesha wafugaji kutambulika katika kijiji na haiwezi kuondoa thamani ya ngozi katika soko.

Katika taarifa ya uendeshaji wa zoezi hilo, chapa ya serikali inadaiwa kuwa haimzuii mfugaji kuweka chapa yake binafsi lakini anapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa ili kusiwepo madhara ya uharibifu wa ngozi.

Baada ya kukamilika zoezi hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema inaandaa mpango wa kuwawezesha wafugaji kufuga kwa tija ili wanufaike na kulifikia soko kwa bidha zote zinazotokana na mifugo kwa kuweka miundo mbinu ikiwemo ya majosho.

Zoezi la ufunguzi la upigaji chapa ya taifa limefanyika katika kijiji cha Isebya kata ya Kishinda wilaya humo ambapo zaidi ya Ng’ombe elfu tatu wamepigwa chapa.

Picha na mtandao

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.