Gavana wa Benki kuu Tanzania Florens Luoga amesema muda sio mrefu itaweka kanuni za kuhakikisha fedha zinazotokana na madini zinarudi Nchini kwani wawekezaji walikua wnadanganya kwa sababu ya kuwa na akaunti za benki nje ya nchi na kusababisha fedha kutorudi Nchini.
Taarifa na Salma Mrisho.
Akiwa Mkoani Geita kwa ziara ya siku moja na kutembelea mgodi wa dhahabu wa geita pamoja na maeneo mengine kuangalia hali ya uzalishaji wa dhahabu unavyofanyika.
Luoga amesema kuwa haiwezekani Tanzania kuwa na dhahabu za kutosha halafu hakuna eneo la kuhifadhi dhahabu na kuongeza kuwa hivi karibuni kutakua na kanuni za uhifadhi wa dhahabu.
Uwepo wa masoko ya dhahabu umechangia kupatikana kwa mapato ambapo kuanzia machi 2019 hadi januari 2020 umeshazalisha tani tatu za Dhahabu zenye thamani ya bilioni 362.
Suala la kituo cha kuhifadhi dhahabu nalo limezungumzwa na kuonekana kama changamoto inayowakabili wawekezaji hao ambapo BOT wamesema watakaa na kulifanyia kazi.
Halmashauri ya Mji wa Geita tayari imetenga maeneo ya kimkakati kwa shughuli mbalimbali za sekta ya madini.
Mwisho.