Star Tv

Serikali imemtahadharisha mkandarasi anayetekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kituo cha Daladala Manispaa ya Morogoro kuwa huenda akabomoa na kuanza kujenga upya kwa gharama zake jengo la Utawala linalogharimu kiasi cha shilingi Milioni 400 itakapobainika kujengwa chini ya kiwango.

Habari na  Omary Hussein

Kituo hicho cha Dalalada manispaa ya Morogoro ambachoo utekelezaji wake unagharimu zaidi ya shilingi Bilion 5 ambazo ni fedha za mkopo kutoka benki ya dunia, ukitekelezwa na mkandarasi mzalendo kampuni ya Nandra Engenearing Constractin LTD, ya Jijini Dar es salaam.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Selemani Jafo ambaye amefika kukagua mradi huo wa ujenzi wa kituo cha daladala amesema kuwa wasiwasi wake ni muonekano wa jengo la Utawala ambalo amemsihi mkandarasi kuhakikisha jengo hilo linajengwa vyema na mkandarasi huyo ameaswa kuzingatia makubaliano ya mkataba.  

Katika hatua nyingine akiwa mkoani hapa waziri Jafo amekagua na kuzindua shule mpya ya Mfano kwa shule za Sekondari za serikali nchini, shule ya Sekondari Mji mpya iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilion 1.4.

Awali  baadhi ya viongozi mkoa huo wamesema kupatikana kwa shule hiyo ya Mfano, kutaongeza ushindani katika mitihani ya kitaifa wakitamani shule hiyo kupanda hadhi kuchukua pia wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Shule hiyo ya sekondari ambayo utekelezaji wake umegharimu kiasi cha bilioni 1 na million 400 fedha ambazo ni matunda ya Mradi wa Reli ya kisasa, inatajwa kuwa ndio shule ya mfano kwa shule zote za serikali nchini hususani ngazi ya kata, na utekelezaji wake umezingatia miundombinu ya wenye mahitaji maalum, maktaba ya kisasa na maabara kwa masomo yote ya sayansi.

                                                                                     Mwisho.

 

 

Latest News

KUNDI LA MAI-MAI LAENDELEA KUUTESA MJI WA LUBUMBASHI KWA MAPIGANO.
26 Sep 2020 15:30 - Grace Melleor

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mku [ ... ]

AJALI YA NDEGE YA JESHI LA UKRAINE YASABABISHA VIFO VYA WATU 22.
26 Sep 2020 08:31 - Grace Melleor

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa na abiria watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. [ ... ]

BAH N'DAW KUAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO NCHINI MALI.
25 Sep 2020 09:24 - Grace Melleor

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.