Star Tv

Mama mmoja aitwaye Neema Joseph mkazi wa kijiji cha Burungu wilaya ya Musoma Mkoani Mara ameliwa na Mamba wakati akioga ndani ya Ziwa Victoria majira ya saa nne usiku katika ufukwe wa Bulungu.

Habari na Sadick Hunga ...

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polis Daniel Shillah wakati akizungumzia tukio hilo amesema mama huyo baada ya kumaliza kufanya biashara yake ya kuuza chakula alikwenda kuoga pembezoni mwa ziwa Victoria na ndipo alipokutwa na masahibu hayo.

 “Lakini katika kuoga kwenye ufukwe aliweza kukatwa na mamba na kupoetza Maisha juhudi za kutafuta mabaki ya mwili wa mama huyo zinaendelea”;ACP Daniel Shillah – Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara

Baadhi ya wakazi wa eneo wakizungumzia tukio hilo wameiomba serikali kutoa elimu juu ya ongezeko la wanyama wakali pembezoni mwa ziwa hilo na kuwaelimisha wananchi kutooga ziwani kwakuwa ni hatari endapo viumbe wa majini wa aina hiyo wanapokuwepo ndani ya maji.

Wakati hilo likijiri jeshi la polisi pia  limefanikiwa kuukamata mtandao wa wauza madawa ya kulevya wanane wakiwa safarini kwenda jijini Mwanza kuyauza.

Kamanda Shillah Ametoa wito kwa wananchi kuepuka kutenda vitendo vya uhalifu kutokana na doria zinazoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

                                                                       Mwisho.

Latest News

KUNDI LA MAI-MAI LAENDELEA KUUTESA MJI WA LUBUMBASHI KWA MAPIGANO.
26 Sep 2020 15:30 - Grace Melleor

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mku [ ... ]

AJALI YA NDEGE YA JESHI LA UKRAINE YASABABISHA VIFO VYA WATU 22.
26 Sep 2020 08:31 - Grace Melleor

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa na abiria watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. [ ... ]

BAH N'DAW KUAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO NCHINI MALI.
25 Sep 2020 09:24 - Grace Melleor

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.