Star Tv

Serikali inakusudia kuzifuta ofisi za ardhi za kanda na kuanzisha ofisi za mikoa ambazo zitashughulikia masuala yote ya ardhi ili kuondoa urasimu na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Habari na Laudence Simkonda.

Idara ya ardhi ambayo ni miongoni mwa idara za serikali zinazotajwa kulalamikiwa zaidi na wananchi kutokana na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro ya mara kwa mara ya ardhi.

Hayo yamejiri baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi alipokutana na maafisa wa idara ya ardhi kutoka mikoa saba ya nyanda za juu kusini waziri Lukuvi ameeleza nia ya serikali ya kuvunja ofisi hizo za kanda.  

Waziri Lukuvi amesema kanda nane ziliozopo atazifuta hivyo kutakuwa na uwakilishi wa kila mkoa  na wizara inatarajia kuanzisha rasmi ofisi za ardhi za mkoa, kwa ajili ya kuondoa urasimu na kuondoa kero ya mfumo uliopo.

Pia  amekemea vitendo vya rushwa vinavyoendelea kwenye ardhi na amewataka wafanyakazi waliopo ndani ya wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Aidha, lengo la kukutana kwa maafisa hao wa idara ya ardhi kutoka mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini ni kujifunza mfumo mpya wa kielektoniki kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ardhi .

Waziri Lukuvi pia amewasisitizia maafisa wa idara ya ardhi kutumia ipasavyo mafunzo waliyoyapata kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato, huku akituma salamu kwa wakwepa kodi ya ardhi na majengo.

                                                                              Mwisho

Latest News

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

KIJANA WA MIAKA 20 AMTEKA NYARA BABA YAKE NA KUDAI ALIPWE FIDIA.
21 Jan 2021 16:09 - Grace Melleor

Polisi wamemkamata mwanamume mmoja aliyejulikana kwa jina la Abubakar Amodu mwenye umri wa miaka 20, ambaye alipanga nja [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.