Star Tv

Mawakala inayotekeleza zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole mkoani Njombe wameitupia lawama mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA kwa kuchelewa kukamilisha zoezi hilo kwa wakati. 

 Habari na Dickson Kanyika.

Zoezi la usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za vidole linalosimamiwa kisheria na  mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA ilivyomtaka kila mmoja kuhakikisha amesajili kadi ya simu kwa mtindo huo.

Njia hii ni  moja ambayo inaelezwa itasaidia mamlaka husika kudhibiti uhalifu wa kimtandao, lakini pia kuwabaini wahusika kwa urahisi zaidi pindi uhalifu wa kimtandao unapofanyika.

Imeelezwa kuwa kucheleweshwa huko  kumeleta changamoto kubwa kwa wananchi ambao wanahitaji kutambuliwa laini zao za simu kwa alama za vidole, kwani wengi wao wamejikuta wakipoteza gharama nyingi  kwa kusafiri kutoka vijijini hadi mijini kufuata huduma hiyo wakihofia kusitishiwa mawasiliano kama serikali ilivyowaonya kwa kuongeza muda wa siku 20 tu kutoka januari mosi hadi January 20 mwaka huu.

Baadhi ya wananchi wamesema muda uliotolewa hautoshi ukilinganisha na mwenendo wa zoezi  la usajili linavyoendeshwa.

Baada ya malalamiko yote hayo ya wananchi mratibu wa NIDA mkoa wa Njombe ambapo amebainisha kuwa  hakuna tatizo kwa mamlaka ya mawasiliano kuzorotesha zoezi hilo la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kama ambavyo  raia wanailaumu mamlaka hiyo kwa kutokupata muafaka wa mawasiliano ikiwa laini zao zitazimwa.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imeweza kubainisha kuwa laini ambazo hazijakamilisha usajili zitazimwa ifikapo saa sita usiku wa kuamkia January 21 mwaka huu huku wananchi walio wengi  wakimlilia Rais Magufuli kuwaongezea Muda.

                                                                                                               Mwisho.

Latest News

KUNDI LA MAI-MAI LAENDELEA KUUTESA MJI WA LUBUMBASHI KWA MAPIGANO.
26 Sep 2020 15:30 - Grace Melleor

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mku [ ... ]

AJALI YA NDEGE YA JESHI LA UKRAINE YASABABISHA VIFO VYA WATU 22.
26 Sep 2020 08:31 - Grace Melleor

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa na abiria watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. [ ... ]

BAH N'DAW KUAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO NCHINI MALI.
25 Sep 2020 09:24 - Grace Melleor

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.