Star Tv

Aliyewahi kuwa  katibu  wa baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mzee Samuel Kasori amesikitishwa na hatua ya serikali ya kukitelekeza chuo cha utafiti wa kilimo na  mifugo Uyole jijini Mbeya, ambacho kilianzishwa na mwalimu Nyerere kwa misingi maalumu ya kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

Mzee Kasori amesema kuwa kwa mara ya kwanza alifika chuoni hapo akiwa na mwalimu Nyerere mika ya 1990.

Matarajio yake ilikuwa ni kutaka kuona miundombinu ya  chuo hicho cha kilimo Uyole kikiendelea kung’aa na kufanya kazi zilizo kusudiwa na baba wa taifa.

Lakini uchakavu wa majengo na miundombunu mibovu ya barabara ndani ya chuo hicho ilimuhuzunisha katibu Kasori ambaye ni mwalimu Nyerere.

“Akili zetu katika karne ya 21 unaaamua kudhoofisha usafiri wa reli, bandari, pamoja na vituo vya utafiti n ahata elimu kwa ujumla”; Samuel Kasori aliyewahi kuwa katibu wa Mwl. Nyerere.

Baada ya kukutana na watumishi wa chuo hicho aliweza kuwaeleza kwamba  dhamira ya baba wa taifa kuweka alama ya taasisi hiyo kwa kukianzisha ilikuwa ni kuweza kujitegemea katika chakula na ndio maana chuo hicho kilianzishwa.

Ukosefu wa bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo umetajwa kuwa miongoni mwa kikwazo kinachowakwamisha watafiti kutafiti na kukuza teknolojia ya mifugo hapa nchini.

Chuo cha utafiti wa kilimo na mifugo Uyole ni moja ya taasisi za serikali zilizoashwa maalumu kwa ajili ya kutafiti na kukuza technologia ya kilimo na mifugo hapa nchini.

Mwisho.

 

 

 

 

Latest News

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

KIJANA WA MIAKA 20 AMTEKA NYARA BABA YAKE NA KUDAI ALIPWE FIDIA.
21 Jan 2021 16:09 - Grace Melleor

Polisi wamemkamata mwanamume mmoja aliyejulikana kwa jina la Abubakar Amodu mwenye umri wa miaka 20, ambaye alipanga nja [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.