Star Tv

Kijana Devenja Kibotuo (35) mkazi wa Kijiji cha Uchau kusini Wilaya ya Moshi,mkoani Kilimanjaro  anadaiwa kufukua kaburi la mtoto wa dada yake aliyezikwa miaka 16 iliyopita kisha  kuotesha mgomba kwenye kaburi hilo. 

Kijana huyo anadaiwa kufukua kaburi la mtoto wa dada yake  aitwae Juliana Andrea aliyezikwa mwaka 2004 ambae alifariki akiwa na umri wa miezi tisa huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.

Wahenga walisema damu nzito kuliko maji ila kwa  kijana huyu imekuwa kinyume,tukio hilo ambalo limezua sintofahamu baada ya ndugu kujua kaburi limefukuliwa  wanasema walikuta sanda ikiwa juu ya kaburi huku wakikosa majibu kutoka kwa ndugu yao aliyefukua kaburi kisha kupanda mgomba.

Mmoja wa wana familia alieleza kuwa kwa mila na taratibu zao inapotokea kaburi limefukuliwa ni lazima zifanyike mila kwa ajili ya kulifukia na endapo haitafanyika hivyo itakuwa na madhara kwa familia.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro James Manyama amethibitisha kumshikilia kijana Devenja baada ya kufukua kaburi hilo mtoto wa dada yake bila kuwa na kibali cha mahakama.

Jeshi la polisi kutoka mkoani humo limesema litafukua kaburi hilo siku ya leo jumatatu baada ya kupata kibali cha mahakama ili kujua kama kuna masalia ya mifupa itakuwa imechukuliwa na kijana huyo pamoja na kushirikisha idara ya afya kujua kama kijana  aliyefukua kaburi hilo ana akili timamu.

Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.