Wakazi wa Kijiji cha Tatwe wilayani Rorya mkoani Mara wamekumbwa na maporomoko ya ardhi ambayo yamesababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Mvua hizo zimeelezwa kusababisha hasara kubwa kwani idadi kubwa ya ekari za mashamba na baadhi ya mifugo pamoja na kuathiri kaya kumi zinazohitaji msaada wa hali na mali.
Kutokana na mvua hizo kuleta athari kubwa katika kijiji hicho kaya kumi ambazo zimeathirika zinaomba kupatiwa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula pamoja na kuhamishiwa kwenye eneo salama ili kuepuka maafa.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sang'ombe kijiji cha Tatwe Wilayani Royra Mkoani Mara Kevin Chacha amesema.“Naomba serikali isaidie hawa wakazi wa Kijiji changu kwa mbinu zozote ambazo wataweza kuwasaidia, kama ni chakula wapewe”
Lameck Airo ambaye ni mbunge wa jimbo la Rorya akiongozana na mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Charles Ochele wamefika katika kitongoji cha Sang'ombe kilichoko katika kijiji cha Tatwe ili kujionea hali halisi ya tukio hilo ambalo halijawahi kutokea na kuwapa pole wakazi waliofikwa na janga hilo.
“Mimi toka nimezaliwa sijawahikuona tukio la jabu Tanzania nzima kama nililoliona leo kama chanzo ni maji yameweza kulipuka na baada ya kulipuka ikasababisha mto mkubwa kama huu ni maajabu na nitawachangia wananchi milioni moja”
Maporomoko hayo ambayo ni ya kwanza kutokea katika kijiji cha Tatwe Wilayani Rorya na yametengeneza korongo lenye urefu wa zaidi ya kilometa mbili na kuacha Historia kwa wakazi wa Kijiji hicho cha Tatwe.
Mwisho