Star Tv

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO mkoa wa Pwani Martin Maduu kuangalia namna ya kuwaunganishia umeme wananchi wanaokuwa wametoa nusu ya fedha zao ili waweze kukatwa wakati wa kununua luku na hivyo kuanza kunufaika mapema badala ya kusubiri hadi wanapomaliza kulipia.

 

Naibu waziri Mgalu amewasha Umeme katika Kijiji cha Migudeni Kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo Umeme huo utasaidia kusukuma maji katika kisima kilichopo na wakazi wa hapo kunufaika na Umeme.

 

Aidha Mgalu amekabidhi Cement mifuko 50 kwaajili ya Ujenzi wa shule ya msingi kiromo ambayo ni shule mpya.

 

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Shukuru Kawambwa amemshukuru Naibu waziri pamoja na waziri wa kwa kusimamia masuala ya Umeme Tanzania nzima na hasa mkoa wa Pwani.

 

                                                                     Mwisho

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.