Star Tv

Baadhi ya wazazi katika shule ya msingi Azimio A jijini Mwanza wamegoma kutoa mchango wa shilingi 500 kuwezesha watoto wao kula chakula shuleni licha ya kuwa baadhi ya watoto wanatajwa kutoroka mara kadhaa katika muda wa mapumziko kwenda kuosha vyombo kwenye magenge ili waweze kupatiwa ukoko na masalia ya vyakula .

Taarifa na  Projestus Binamungu.

Mkutano huo wa mwisho wa mwaka katika shule ya msingi Azimio A ambapo mada iliyoleta utata ni wazazi kuchangia shilingi 500 kwa ajili kuwezesha watoto wao kupatiwa chakula pindi wawapo shuleni.

 Mkutano huo ni wa mara ya tatu kuitishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo  Ratwifu Kalokola ukilenga kuwapa elimu wazazi juu ya  kwanini watoto wao wanastahili angalau kunywa uji  pindi wawapo shuleni kitu ambamcho hakikupata muafaka wa hela hiyo kuchangishwa kutoka kwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.

Wazazi wanasema hilo ni wazo zuri lakini wao ni wenye uwezo duni ambao kwao mtoto mmoja kutumia shilingi 500 peke yake ni sawa na anasa.

Jambo hilo la watoto kula shuleni hapo limekataliwa na wazazi walio wengi wengi kwa mwavuli wakutaja kile walichokiita umasikini ambapo imebainishwa kuwa waathirika wakubwa ni wanafunzi wa madarasa ya chini ambao umri wao ni kuanzia miaka tisa kushuka chini.

Wazazi hawakuwa tayari kutoa mchango wa shilingi 500 ili watoto wao wapate angalau wali maharage shuleni  na badala yake wakasema wako radhi kutoa mchango wa shilingi 200 mpaka 1000 kwa watoto ili wanunue maembe,ubuyu ufuta na vitumbua.

Pia imebainika kuwa maisha ya baadhi ya wenyeji wa Igogo si ya kibwenyenye kama ilivyofikiriwa  japo eneo hilo ni miongoni mwa maeneo kongwe ya jiji la mwanza.

Sehemu kubwa ya watoto katika eneo hilo wanalelewa na bibi ama mzazi wa upande mmoja, hatua inayotajwa kuwa ni ngumu kuwashawishi kulikubali wazo la mwalimu Ratwifu Kalokola la watoto kula shuleni.

Hata hivyo si wote wanaunga mkono watoto kushinda na njaa na hasa watoto wadogo wa madarasa ya awali mpaka darasa la nne hali inayoonyesha ukinzani kwa pande mbili za wazazi na ni Dhahiri kuwa wazo la mwalimu Kalokola pamoja na uongozi wake limekwamishwa kutokana na mtazamo hasi wa wazazi..

 Mwenyekiti wa kamati ya shule anasema kwa hatua hiyo hana budi kuandika maandiko kuomba mashirika na wahisani kuiwezesha shule yake ili iweze kupatiwa msaada wa chakula.

 Kukosekana kwa chakula shuleni kumetajwa mara kadhaa kuathiri ukuaji wa mtoto na kiwango kizuri cha ufaulu na hasa kwa watoto wadogo ambao mwili na ubongo ni wenye uhitaji mkubwa wa chakula.

 Aidha, Kwa maamuzi hayo ya wazazi ni dhairi kuwa mwaka 2020 mwezi mmoja tu kuanzia sasa watoto hawa watashinda njaa muda wote wawapo shuleni.

 

                                                                                          Mwisho.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.