Star Tv

Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Kibaha mkoani Pwani Bi.Assumpter Mshama amemkamata Msimamizi wa kiwanda cha Sunda chemical Fiber Limited Bwana Yaung kwa kutokuwa na mikataba ya wafanyakazi na vitendea kazi pamoja na kutokumpatia matibabu mfanyakazi ambaye aliungua mguu akiwa kazini.

 Taarifa na Monica Msomba.

Bi.Mshama amekemea vikali vitendo vya watu wenye viwanda kuwanyanyasa wafanyakazi bila kuwapa stahiki zao  sahihi kama mikataba, Vitendea kazi, na  kuwafanyisha kazi masaa ya ziada bila kulipwa, hivyo kumpeleke msimamizi wa kiwanda hicho  Mr Yaung kituo cha Polisi Mlandizi kwenda kutoa maelezo kina.

Naye kijana Shebi Juma Rashid ambaye aliumia Mguu akiwa kazini  kiwandani hapo  kwa kuungua na maji ya moto ameelezea namna ilivyokuwa.

“Mimi sikuipenda nikamwambia kiongozi wangu kuwa haya maji ni ya moto yanatakiwa kutolewa kwa mashine na sio kwa mikono, kiongozi akakataa akasema fanya hivyohivyo namimi nilikuwa sina nguvu yakukataana  kwa kawaida kiongozi wetu akikwambia fanya kazi usipofanya anakufukuza hivyo nikafanya”.Anasema Juma.

Kwa upande wao wafanyakazi wakiwa kiwandani  nao wakapata fursa ya Bi.Mshama changamoto wanazokumbana nazo hapo kazini ikiwemo maji wanayotumia si salama, na hawana muda wakutosha wakupumzika.

                                                                                       Mwisho. 

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.