Star Tv

Anguko la baadhi ya benki nchini limetajwa kusababishwa na masharti magumu ya uendeshaji wa taasisi za kifedha yaliyowekwa na benki kuu “BoT” likiwemo sharti la kianzio cha mtaji linalodaiwa kuzipa wakati mgumu benki za wananchi kupata leseni ya kufanya kazi.

 Taarifa na Oliver Motto:-

Wanahisa wanaomiliki benki ya wananchi Mucoba PLC – wamesema kufa kwa benki nyingi za wananchi sababu ni masharti magumu yaliyowekwa na benki kuu “BoT” likiwemo sharti la benki za kijamii kuwa na mtaji usiopungua kiasi cha shilingi Bilioni mbili - jambo linalotazamwa na wanahisa kama ni miongoni mwa vikwazo kwa benki zao

Wananchi Wilayani Mufindi kwa kiwango kikubwa ndiyo wametajwa kuwa waanzilishi na wamiliki wa Benki ya wananchi Mucoba – benki ya kijamii inayoendeshwa kwa hisa za wakulima na wafanyabiashara wadogo na wakati, wananchi hao wameiomba benki ya BoT iwapunguze masharti ili benki za wananchi ziweze kuendelea.

Omary Msuya ambaye ni  afisa wa benki kuu - dawati la BoT lililopo katika benki ya Mucoba, ametoa ufafanuzi juu ya hili kwa kusema kuwa.“Baada ya vitu kukaa  sawa na mipangilio yote haya yote yatatatuliwa na gawio mtaweza kulipata hivyo muwe wavumilivu”.Anasema Omari Msuya

Haya yote yamezungumzwa na wanahisa katika mkutano mkuu wa 20 wa mwaka 2019 uliofanyika Mafinga Wilayani Mufindi- ambapo wanahisa walikwama kupata gawio kwa madai ya zuio lililowekwa na BoT.

 

                                                                                                  Mwisho

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.