Star Tv

Wakazi wa kijiji cha Pemba wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wamewataka viongozi wakiwemo Mbunge na Diwani kujitathimini kutokana na viongozi hao kutajwa kushindwa kutatua tatizo sugu  la ubovu wa barabara ambayo ni kikwazo cha kusafirisha mazao yao na kufanya  kuozea mashambani.

 

Ni Safari ya kuelekea kjiji cha Pemba, kijiji ambacho kipo wilayani Mvomero mkaoni hapa, usafiri unaotumika kwa sasa kufikia kijijini hapo ni usafiri wa pikipiki ambao nao unahitaji umakini wa dereva ili kuweza kufika salama.

 

Ubovu wa Miundombinu unahakisi maisha halisi ya watu wa kijiji cha pemba, ambao wao wanaona usimamizi mbovu wa viongozi wao ndio unachangia wao kuishi katika hali ngumi na kushindwa kusafirisha mazao yao.

 

Kijiji hicho kinatajwa kushika nafasi ya Pili kwa kuingizia mapato halmashauri ya wilaya ya Mvomero kutokana na uzalishaji kwa mazao  kwa wingi ikiwemo miwa, Kahawa na  magimbi

Niliweza kuwatafuta viongozi hao wawili kwa njia ya simu ya mkononi akiwemo mbunge na diwani wa kata hiyo  lakini niliweza kufanikiwa kumpata tu diwani ndugu Kimaisi Palasino kujibu tuhuma hizo za wananchi ambaye naye bila kusita anasema mambo hayo yanatokana na siasa na sio barabara pekee..

 

Tatizo hili limeathiri sio tu Maisha ya kila siku bali hata wafanyabiashara wanalalama

 

Uongozi wa kata ya Pemba unakiri uwepo wa changamoto hiyo ya barabara lakini unasema tayari serikali ishatoa fedha kwa ajili ya barabara ingawa  ni ndogo.

 

Kwa upande wake mratibu wa wakala wa barabara vijijini (Tarura) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Mpinzile  anasema wanatambua changamoto wanazokutana nazo wananchi msimu huu wa mvua hasa maeneo ya  wilaya za Mvomero na Kilosa.

Licha ya ubovu wa barabara pia kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mtandao wa simu hatua ambayo inatjwa pia kukwamisha maendeleo ya kijiji hicho cha Pemba

                                           Mwisho

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.