Star Tv

Wizara ya Maliasili na Utalii imekemea tabia ya uvamizi kwa baadhi ya wakazi wanaozunguka hifadhi za taifa ,mashamba ya miti na Mapori ya akiba ambapo wanadaiwa kufanya uharibifu na hivyo kutishia ustawi wa Rasilimali hizo.

Taarifa na Sudi Shabani.

Shamba la miti Buhindi lenye ukubwa wa kilometa za Mraba 21,880 ni miongoni mwa mashaba 23 nchini likiwa na miti ya asili na mingine iliyopandwa.

Licha ya shamba hilo kutoa faida kemkem za kiuchumi lakini ni lenye kukumbwa na changamoto ya uvamizi baadhi ya wakazi wakitajwa kufanya shughuli za kilimo, uvunaji wa mbao usiofuata taratibu sanjari na uchomaji Mkaa.

Upande wa pili wa shilingi mafanikio ya dhati juu ya uwepo wa shamba la Buhindi yanaonekana kwa kuleta faida zenye kuzaa matunda hata kwa wakazi wanaozunguka shamba hilo.

Pia bodi ya wadau wa kupansua mbao katika shamba hilo liliweza kukabidhi bweni la wasichana  ambalo wamelijenga kwa nguvu zao katika shule ya Sekondari Irenza iliyopo halmashauri ya wilaya ya Buchosa Mkoani mwanza,

Bweni hilo liliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 60 kwa michango ya wadau wa shamba la Buhindi ikiwa ni mkakati wa kuunga Mkono sera ya serikali ya kuboresha elimu nchini haswa kwa jamii ya watoto wa kike

 Pamoja na kuthamini sekta ya Elimu Wadau hao pia wamekabidhi vifaa tiba, vitanda na shuka kwa zahanati 10 za vijiji vinavyozunguka shamba hilo. 

 

                                                                                             Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.