Star Tv

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetangaza kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya kiasi cha shilingi trilioni 23.4 sawa na asilimia 70 tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani.

Taarifa na Athuman Mihula.

TRA kupitia kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo Msafiri Mbibo amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati akielezea mafanikio ya TRA tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani huku akieleza kuwa jumla ya kiasi cha shilingi trilioni 58.3 kimekusanywa katika kipindi cha miaka minne ukilinganisha na trilioni 34.9 katika kipindi kama hicho kilichopita…..

Ameeleza kuwa licha ya kuboresha mifumo ya makusanyo ya fedha pia kuanzishwa kwa vyanzo vipya vya mapato sambamba na kuimarika kwa matumizi ya mashine za kieletroniki EFD yamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo……

 “Sababu nyingine iliyopelekea kuongezeka kwa mapato hayo ni kuimarika kwa mashine za kielektroniki ambapo badala ya kuandika stakabadhi kwa mkono sasa zinatolewa kwa mashine na kuimarika kwa muamko wa wananchi kudai risiti pindi wanapofanya manunuzi ..Msafiri Mbibo naibu kamishina wa TRA”

Katika mafanikio hayo, serikali pia imefanyia kazi mapendekezo ya wafanyabiashara kwa kufanya mabadiliko ya sheria kwa kufuta tozo 54 ambazo zilikuwa kikwazo kwa ustawi wa biashara nchini.

                                                                                          Mwisho.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.