Star Tv

Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara imeviagiza vyombo vya dola kuwasaka vijana watatu waliokimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kumchoma mkuki shingoni na kumuua mwalimu Justin Sospeter Ogo wa shule ya sekondari Itiryo.

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Mara Adam Malima akizungumza na vyombo vya hanari ofisini kwake kufuatia kuelezwa juu ya taharuki toka kwa walimu kuhofia usalama wao kutokana na vijana hao kumuua mwalimu mwenzao wakati alipokuwa akiwasindikiza wenzake kwenda kusimamia mitihani.

 Akizungumzia hali hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mara Adam Malima amewataka walimu kuendelea na majukumu yao bila hofu.

 Pamoja na suala hilo Malima amepiga marufuku shughuli zote za tohara mpaka hapo vijana hao watatu watakapopatikana.

Hivi karibuni vijana wanane waliokuwa wakijiandaa kufanyiwa tohara walimpiga mkuki wa shingo Mwalimu Justin Ogo wa shule ya sekondari Ogoo huku wakidaiwa kumvunja mkono mwanafunzi wa kidato cha nne kwa madai ya kuonyesha ujana wao kabla ya tohala.

 

                                                                                   Mwisho

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.