Star Tv

Serikali imesema itahakikisha sekta ya usafiri wa anga nchini inaimarika ikiitaka mamlaka ya ufasiri wa anga nchini TCAA kuongeza uwajibikaji zaidi ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa ubora kama ilivyo kwenye mataifa yaliyoendelea.

 Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa udhibiti wa uchumi na biashara wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA Daniel Malanga, wakati wa mkutano uliowakutanisha kamati maalumu ya usafiri wa anga ya jumuiya ya Afrika mashariki na sekretaieti ya jumuiya hiyo unaokusudua kujadili changamoto zinazokabili mamlaka hizo na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuboresha sekaya ya usafiri wa anga.

 Aidha, TCAA imesema kuwa itahakikisha inaongeza vyanzo vya mapato na kuondokana na kutegemea zaidi mapato yanayotokana na maegesho ya ndege.

 Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamesema kutakuwa  muhimu sana katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi za jumuiya hiyo nakuongeza ufanisi wa huduma za usafiri wa anga Afrika ya mashariki

 Kamati hiyo hukutana kila baada ya miezi sita ikiwa ni muendelezo wa kutatua changamoto na kuweka mikakati kadhaa ili kuhakikisha mamlaka za usafiri wa anga kwa nchi za Afrika mashariki zinaimarika zaidi

 

                                                                                     Mwisho

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.