Star Tv

Jamii imetakiwa kuacha kuwaita watu wenye ualbino majina ya kejeli ambayo yanayowavunjiwa utu na heshima yao.

Wilaya ya Busega inakadiriwa kuwa na watu wenye ualbino 110 lakini changamoto kwa kundi hili ni kuitwa majina ya kejeli ambayo kwa hakika yanawavunjia utu na heshima yao.

Kutokana na hali hiyo imepelekea chama cha watu wenye ualbino wilaya ya Busega, kwa kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii kutoa elimu kwa jamii, kupitia wanafunzi na mikutano ya hadhara lengo likiwa  ni kuondoa dhana potofu kwa jamii kuhusu watu hao wenye ulemavu wa ngozi.

Pamoja na changamoto hiyo inayolikabili kundi hili, lakini jamii wakiwemo wanafunzi wamesema kwa sasa mtazamo ni tofauti, kwani wanawaona wenye ualbino sawa na watu wengine ikilinganishwa na zamani ambapo walikuwa wanaonekana kama mkosi kuwepo kwenye jamii.

Aidha, Hatua hiyo ni mwendelezo wa harakati za kuondoa mtazamo hasi na kutoa uelewa mpana kwa jamii dhidi ya watu wenye ualbino.
      

                                                                        Mwisho

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.