Star Tv

Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza umeunga mkono Hatua ya serikali ya kupiga marufuku ibada  zinazoendeshwa na Diana Bundala anayejiita Mfalme Zumaridi baada ya kubainika ibada hizo zinafanyika kinyume na sheria na taratibu za nchi.

 

Ikiwa bado ni hali ya kushangaza kwa wengi waliosikia na kushuhudia Serikali ikilifungia Kanisa la Mfalme Zumalidi Jijini Mwanza ikidawa ibada na imani za kanisa hilo hazithibiti matakwa ya ukristo.

 Umoja wa makanisa Jijini Hapa unaoundwa na mabaraza ya TEC, CCT na CPCT umevunja ukimya na kutoa tamko rasmi kuiunga Mkono serikali juu ya hatua iliyochukua dhidi ya kanisa hilo.

 Kanisa hilo linadaiwa kutumia usajili wa Kanisa la pentekoste ambapo umoja huu umesema hali hiyo inakwenda kuchafua wakikristo neno kwa wizara ya mambo ya ndani yakwamba hali hiyo ikitokea inachafua wakristo wote.

 Askofu. Philipo Mafuja ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa makanisa jijini Mwanza amesema  “Kama mtu amefika mahala anasema kikristo amepitwa na wakati ni lazima ataumiza hisia za watu wengi”

 Pia Askofu Zenobius Isaya ambaye ni Katibu wa baraza la makanisa ya kipentekoste amesema “Kama mtu amefika mahala alikuwa anajiita Mungu sasa mtu akishajiita Mungu ni kejeli ya kiwango cha juu na ndio maana alikuwa na maneno mengi anasema Mwanza hii hakuna wachungaji kama mimi”

 Novemba 18 mwaka huu, kamati ya Ulinzi na Usalama Ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana walitembelea kanisa hilo na kutoridhishwa  na utaratibu wa uendeshwaji wa ibada na hivyo kufikia hatua ya kulifunga.

                                                                                                     Mwisho.

 

Latest News

MLIPUAJI WA KUJITOA MUHANGA AWAUA WATU SITA MOGADISHU.
04 Jul 2020 16:20 - Grace Melleor

Takriban watu sita wameripotiwa kufariki baada ya bomu kulipuka katika mgahawa mmoja uliopo mji wa kusini wa Somalia wa  [ ... ]

LISSU ATANGAZA KUREJEA NCHINI JULAI MWISHONI.
04 Jul 2020 11:19 - Grace Melleor

Kuelekea Mkutano wa Baraza la Chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Mhe. Tundu Lissu amesema atarudi nyumbani (T [ ... ]

UFARANSA YAMPATA WAZIRI MKUU MPYA.
04 Jul 2020 10:57 - Grace Melleor

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Jean Castex, mwanasiasa asiyefahamika na raia wa nchi hiyo kuwa Waziri Mkuu mp [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.