Star Tv

Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa amesema atawafukuza wakurugenzi wa mamlaka za maji  nchini watakaoshindwa kukusanya vyema  mapato kwani mamlaka hizo zinaendelea kuwa tegemezi kwa seriakali kutokana na uzembe

Ikiwa ni siku ya kwanza katika ziara ya kikazi wilayani Musoma mkoani Mara waziri wa maji Professa Makame Mbarawa ametoa kauli hiyo huku akiwataka wakurugenzi wa mamalaka ya maji nchini walioshindwa kukusanya vvema mapato kujitathuimini kama bado wanafaa .

Akikagua mradi wa maji taka ambao unajengwa mjini Musoma waziri Mbarawa ameridhika na ujenzi wake huku akimtaka mkandarasi kuongeza kasi ili kukamilisha mradi huo.

Serikali wilayani Musoma imemuomba Waziri wa maji kumtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anaweka maji katika vyoo anavyo jingenga ili kupunguza ugonjwa wakichocho.

Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mara kukagua na kuangalia shughuli zinazotekelezwa na watendaji wa wizara hiyo.

                                                                                                    Mwisho.

 

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.