Star Tv

Wananchi wa kata tatu  za Matambalale ,Namikulo  na Namileme wilayani Ruangwa mkoani Lindi wamelipwa fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4 ili kupisha mradi mkubwa wa uchimbaji madini aina ya Bunyu

Mgodi huo  unaomilikiwa na  Lindi jumbo ni miongoni mwa migodi sita ya uchimbaji madini aina ya Bunyu wilayani humo .

Baadhi ya wananchi waliolipwa fidia ili  kupisha uchimbaji huo wameiomba serikali iwape kipaumbele  cha kupata ajira pindi mgodi utakapoanza kufanya kazi

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashimu Mgandilwa   amewataka wakazi wa wilaya hio kujitokeza kwa wingi  kuchangamkia fursa pindi watapo tangaza nafasi za ajira

Mgodi  huo wa uchimbaji madini aina ya Bunyu  utakapo kamilika unatarajiwa kuajiri zaidi ya  watu elfu tatu

Mwisho

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.